Na Sabiha Keis, Zanzibar Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali amesema ongezeko la migogoro ya Ardhi nchini linasababishwa na baadhi ya wananchi kununua Ardhi kwa kutofuata sheria na taratibu zilizowekwa. Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Bajeti kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2022 kwa kamati ya Mawasiliano,Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi huko katika ukumbi wa Wizara hiyo Maisara, Unguja. “Asilimia 80 ya migogoro ya Ardhi inatokana na mauziano ya wananchi kuuziana ardhi kinyume na sheria, na hao wanasheria ndio balaa, kiwanja kimoja kinauzwa mara mbili hata tatu, afadhali hata masheha wakihusishwa wajua kama kiwanja hichi kimeshauzwa “ Alisema Waziri Rahma. Alieleza kwamba mbali na ununuzi huo wa Ardhi usifuata sheria lakini pia ujenzi holela usiozingatia mipaka halisi ya eneo husika umekua ukichangia kuwepo kwa migogoro hiyo ambapo Wizara yake imejipanga kwa sasa katika kudhibiti hali hiyo. Waziri Rahm...