NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MADEREVA na wananchi wanaotumia barabara ya Ole-Kengeja, iliyofunguliwa mwaka 2020 na aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Dk. Ali Mohamed Shein, wamefurahia baada ya zoezi la uwekaji wa alama za barabarani kuanza . Walisema awali, barabara hiyo iliyofunguliwa miaka minne sasa, haikuwa na alama za barabarani, jambo ambalo lilikuwa likiwapa ukakasi, wanapokuwa barabarani. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema kwa sasa wamefurahishwa na uamuzi wa serikali wa awamu ya nane, chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuitaka wizara husika, kuiwekea alama barabara hiyo. Walisema kuwa, kukosekana kwa alama za barabarani, kulikuwa kunatishia maisha yao na watembea kwa miguu, kutokana na kukosekana la alama hizo muhimu. Mmoja kati ya madereva hao, Mohamed Khamis Hasnuu alisema, walikuwa wakipata shida hasa kwa wao wageni wa barabara hiyo, jambo ambalo lingeweza kusababisha ajali. ‘’Hujui wapi kuna skuli, soko, hospitali, mpindo na muunganiko ...