NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR@@@@ MKUU wa mkoa wa mjini Magharibi Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa , amekitaka chuo kikuu cha taifa Zanzibar ( SUZA) kuendelea kuandaa mashindano ya waandishi chipukizi, ili kuwapima uwezo wao katika kada hiyo. Ameyasema hayo, katika hafla ya kuwatunuku vyeti na zawadi washindi wa shindano la waandishi chipukizi, katika chuo cha SUZA kampasi ya Kilimani. Alisema , fani ya uwandishi wa habari ni kada nyeti sana, hivyo ni vyema wanafunzi wakasoma na kufanya kazi kwa bidii, kwani kumeibuka wimbi kubwa la watu wanaojiita waandishi bila ya kuwa na sifa ya uaandishi au bila ya kusomea. “ Siku hizi kumeibuka wimbi la waandishi makanjanja na wao wanajiita waandishi wa habari, wakati hawajasomea hata cheti katika habari na kuichafua kada hii kwa kwenda kinyume na maadili ya uwandishi,”alisema. Aidha alisema kuwa, kwa kupitia mashindano kama hayo, watapatikana wandishi wazuri na wajuzi wa lugha, kwani ili uwe m...