Skip to main content

Posts

Showing posts from March 3, 2024

''PUNGUZENI MATUMIZI YA KARATASI KWA SHUGHULI ZA KIOFISI' MHANDISI ZENA

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WATENDAJI wa taasisi kisiwani Pemba wametakiwa kuacha tabia ya kutumia makaratasi kwenye shughuli zao za kiofisi na badala yake waendelee kutumia mfumo wa kidigitali, ili kuwarahisishia katika utendaji wa kazi zao za kila siku. Akifungua mafunzo ya mfumo wa vibali vya safari za nje ya nchi (ZanVibali), leo Machi 4, 2024 Chake chake Pemba, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandis Zena Ahmed Said alisema, mfumo wa kidigitali ni rahisi na mtumishi atapata kibali kwa haraka. Alisema kuwa mfumo huo ni muhimu sana kwani kutakuwa na uwazi na uwajibikaji, Serikali itaona fedha zote za gharama zitakazotumika kwenye safari pamoja na kurahisisha upatikanaji wa vibali kwa watumishi hao ambapo wakitumia makaratasi huchukua mda mrefu. "Tumeweka mfumo huu kwa ajili ya kuleta tija kwetu kwa sababu mfumo wa makaratasi una changamoto nyingi, hivyo huu utaturahisishia kila kitu na utapata kibali kwa urahisi zaidi pasi na kikwazo chochote," alisem