NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa kuzingatia ulinzi na usalama wao kwanza ,wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa vayama vingi nchini. Akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari, huko katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani Chake chake Pemba, mkufunzi wa mafunzo hayo Mwandishi Maryam Nassor ambae amejengewa uwezo na Umoja wa vilabu vya waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) . na yeye kutakiwa kuipeleka elimu hiyo kwa waandishi wengine Mkufunzi huyo, amesema kuwa, ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari unaanza na mwandishi mwenyeye , hivyo kuwataka waandishi hao kuwa makini wanapotimiza majukumu yao. “ Waandishi wa Habari lazima Kujifunza kusoma mazingira kwa haraka (kama vile maandamano au machafuko) ili kubaki salama wakati munatimiza majukumu yenu” Amese...