NA HAJI NASSOR, PEMBA::::
MKURUGENZI
wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ Harusi Miraji Mpatani,
amewakumbusha wananchi kuwa, njia pekee ya kumaliza matendo ya ukatili na udhalilishaji,
dhidi ya wanawake na watoto, ni wahanga kutokubalia kurubuniwa kwa fedha au ahadi
ya ndoa.
Alisema, mfumo uliopo sasa
kwa wadhalilishaji wakiona wazazi wa muhanga anamsimamo wa kufikisha na
kuisimamia kesi ya mtoto wake, watuhumiwa huanza kutoa ahadi za ndoa na fedha,
ili kuzilainisha kesi hizo.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi kwa njia ya simu leo Novemba 18, 2022 kuelekea siku 16 za kupunga ukatili n
audhalilishaji, Mkurugenzi huyo alisema, tayari zipo kesi kadhaa ambazo
zimeshafikisha mahakamani, na hukosa hatia kutokana na wazazi kukubali kurubuniwa.
Alileza kuwa, wakati huu wa
kuelekea siku 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto, ni
vyema jamii, ikamka na kutetea haki za watoto waliodhalilishwa.
Mkurugenzi huyo alifafanua
kuwa, ikiwa tayari mtoto ameshadhalilishwa, kwa mzazi au mlezi kuchukua fedha
au kitu chengine cha thamani ili kuiua kesi hiyo, ni kumuongezea maumivu mtoto
wake.
‘’Wanaharakati tukiwemo sisi
Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ kwa sasa tumo kwenye kampeni na
ukumbusho maalum, ndani ya siku 16 za kupinga ukatili, kwa jamii kuwa makini na
mbinu chafu za wadhalilishaji,’’alieleza.
‘’Naamini kama jamii
ikiendelea kupata elimu, ushauri na msaada wa kisheria, wanaweza kuona athari
ya kuzifanyia sulhu kesi za udhalilishaji,’’alieleza.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo, amewakumbusha wasimamizi wa haki wakiwemo majaji, mahakimu, waendesha mashtaka, Polisi na wengine kuendelea kutumia weledi wao katika uendeshaji a usimamizi wa utoaji wa haki wa kesi mbali mbali.
Akizungumzia kuhusu siku 16
za kupinga ukatili na udhalilishaji, Mkurugenzi Harusi, amesema ni wakati kwa
jamii kuendelea kufuatilia vyombo vya habari, ili kuongeza elimu ya maarifa.
‘’Kipindi hichi ni kizuri
kwa jamii, kusikiliza vyombo vya habari, ili kuongeza ujuzi wa namna bora ya
kupambana na matendo ya ukatili na udhalilishaji,’’alifafanua.
Hivi karibuni Mkurugenzi wa
Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’ Nassor Bilali Ali,
alisema kila mmoja akitimiza wajibu wake, matendo hayo yataondoka.
Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba
Mattar Zahor Massoud, amewakumbusha masheha, wasijiingize kwenye kusimamia
sulhu ya mtendo hayo.
‘’Sheha ambae atajiingiza
kwenye matendo hayo, na kuyafanyia suluhu, basi mwenyewe andike barua ya kuacha
kazi, kabla sijagundua,’’alisisitiza.
Mzazi ambae mtoto wake wa miaka
11 alibakwa na Khamis Chuma ‘soda’ miaka 76 mjini Chake chake,
alisema matendo hayo kama sheria ya adhabu ya kifungo cha maisha haikutekelezwa,
yanaweza kuendelea.
Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ambacho kimeanzishwa mwaka 1992, malengo yake makuu ni pamoja na kutoa
msaada wa kisheria, kwa wazanzibar bila malipo, ushauri, na elimu ya kisheria
kwa watu hasa maskini.
Mwisho
Comments
Post a Comment