NA HAJI NASSOR, PEMBA WAJAWAZITO wa shehia za Mwambe, Kengeja, Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wameomba kufanyiwa matengenezo ya dharura barabara zao, ili zipitike kwa utulivu wakati wote. Walisema, wamekuwa na changamoto ya usafiri kwa salama, kutokana na barabara zao kuharibika kwa kuwepo mashimo yenye kina kirefu. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, walisema wakati umefika sasa kwa mamlaka husika kuwaonea huruma, kutokana na barabara wanazozitumia kuchakaa. Asha Amini Hilali wa Mwambe alisema, baarabara yao, sasa imekuwa tishio hata kwa garia ya aina gani, kwa kuwepo mashimo yanayohatarisha usalama wao. ‘’Wakati mwengine sisi wajawazito tunalazimika kwenda hospitali ya rufaa ya Abdalla Mzee, lakini wasisi ni kupata mitikisiko kwa ubovu wa barabara,’’alisema. Nae Hamida Machano Makame, alisema mwanzoni mwa mwaka huu, alijifungulia ndani ya gari eneo la Mahuduthi, baada ya gari aliyokuwa akipelekewa hospitali kuingia shimoni na kuka