Na Haji Nassor, PEMBA “Moto ni mtu aliechini ya miaka 18’’ ndivyo sheria namba 6 ya mtoto ya mwaka 2011 ya Zanzibar inavyotoa tafsiri ya nani mtoto. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, yenyewe imeridhia kuwa mtu hatoweza kupiga kuram kama iwapo hatotimizia masharti yaliopo likiwemo la kufikia umri wa miaka 18. Nayo katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imekwenda mbali zaidi kwamba mtu hatochaguliwa kuwa rais kama hajatimiza umri wa miaka 40. Huku taifa la Tanzania likifatua katiba mpya, hata rasimu ya awali ya katiba hiyo iliotolewa Juni 3 mwaka 2013, pamoja na mambo mengine, imerudi ikitaja umri wa miaka 18 ndio wa mtu uzima ndani taifa hili. Tafsiri hii, imekuwa ikiiumisha kichwa jamii ya Zanzibar ambayo asilimia 99, imekuwa ikifuata Imani ya dini ya kiislamu na kuwepo kwa tofauti kubwa. Ingawa tasfsiri ya nani mtoto huja kutokana na mazingira yake, na ndio maana kumbu kumbu zinaonyesha kuwa hata...