NA HAJI NASSOR, PEMBA:::- MKUU wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, leo Juni 11, 2022 ameungana na vilabu vitatu vya mazoezi kikiwemo cha Gombani Fitness Club, na wadau wengine wa haki za mtoto wakiwemo TAMWA, kwenye matembezi maalum ya kuelekea kilele cha siku ya mtoto wa Afrika, hapo Juni 16, mwaka huu. Mkuu huyo wa mkoa, akiongozana na vilabu hivyo vya mazoezi, walianza matembezi yao Polisi Madungu na kumalizia uwanja wa michezo Gombani wilaya ya Chake chake. Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, pia yaliohudhuriwa na wakuu wa wilaya za Chake chake na Mkoani, Mkuu huyo wa mkoa, aliwataka wanamazoezi hao, kuwa wazazi wema kwa watoto wao. Alisema, wapo baadhi ya wazazi wamekuwa wakijitoa mishipa ya fahamu, kwa kuwabaka watoto wao wa kuwazaa, jambo linalosikitisha. ‘’Kwanza nianze na nyinyi, muwe baba na mama wema kwa watoto wenu, maana sasa hali imekuwa ikitisha kwa majanga wanayofanyiwa watoto wetu,’’alieleza. Hata hivyo, amesema wakati ...