NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SHAHIDI nambari 14 kwenye kesi ya mauwaji, ambae ni Daktari wa hospitali ya Vitongoji Chake chake Pemba Ali Juma Ali, amedai mahakamani kuwa, baada ya uchunguzi alibaini kuwa, mjeruhiwa alishambuliwa kwa vitu vyenye cha kali na silaha mfano wa marungu. Alidai kuwa, wakati akiwa kazini kwake hospitalini hapo, Septemba 21, mwaka 2021, alimpokea mjeruhumiwa Suleiman Said Saleh (55) akiwa katika hali mbaya. Shahidi huyo akiongozwa na Wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Ali Amour Makame, mbele ya Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Ibrahim Mzee Ibrahimu, alidai kuwa uchunguuzi ukabini kuwa kina cha jeraha la kichwani ni nchi nne kwa upana na urefu nchi mbili. Alidai kuwa, jeraha jingine ambalo lilikuwa bega la mkono wa kushoto, lilikuwa na nchi tatu kwa urefu na kina cha kwenda chini likuwa nchi mbili. Akiendelea kuongozwa na Wakili wake, shahidi huyo alidai kuwa, wakati anamfanyia uchunguuzi, alibaini pia mkoja wake wakati ukitoka...