NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ WANANCHI wa kijiji cha Tundaua shehia ya Kilindi wilaya ya Chake chake, wamesema hawakatai uwekezaji katika maeneo yao, wanachotaka ni kushirikishwa kila hatua, kuelekea uwekezaji huo. Walisema, kwa sasa wamekuwa wakiona uwekaji wa vikuta ‘bacons’ pembezoni mwa bahari, ndani ya maeneo wanayolima mihogo, mpunga na mboga mboga, bila ya taarifa yoyote kutoka serikalini. Wakizungumza na waandishi wa habari, kufuatia uwepo wa vikuta hivyo, kwenye eneo wanaloendesha kilimo, walisema kinachowasikitisha ni kukosa taarifa, juu ya aina ya uwekezaji huo. Walieleza kuwa, hawajapata taarifa kutoka kwa sheha wao, wala kiongozi mwingine yoyote, na kuwaacha njia panda juu ya zoezi ambalo, limeshakamilika la uwekaji wa vikuta. Mmoja kati ya wananchi hao Makame Haji Makame, alisema ingawa wao hawajakwenda kulalamikia jambo hilo kwa sheha wao, lakini na yeye hajaita kuwapa taarifa zozote. Alisema kama ni suala la uwekazaji, walifikiria kuwa, wengeitwa kwenye ...