NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ CHUO cha Utawala wa Umma Zanzibar ‘IPA’ kimegundua sababu mbali mbali, zinazowafanya watumishi wa umma, kuhama sehemu moja kwenda nyingine, ikiwemo mabadiliko ya sayansi na teknolojia. IPA imegundua sababu nyingine kuwa ni, miundo ya kiutumishi, maslahi na ndoa kwa watumishi wanawake na wanaume, kwa kumfuata mwenzake sehmu alipo kimakaazi. Hayo yameelezwa leo Disemba 8, 2023, na Mkuu wa Divisheni ya Utafiti na Ushauri Elekezi kutoka ‘IPA’ Haji Jumbe Haji, wakati akizungumza kwenye uwasilishaji wa matokeo ya awali wa tafiti nne walizozifanya, kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Chuo, hicho mjini Chake chake. Alisema, sababu hizo na nyingine, zinazowafanya watumishi wahame kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakati mwingine huathiri mtiririko mzuri wa kazi za sekta ya umma. Alisema, tafiti hizo ambazo walizifanya katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, zilichukua takriban miezi sita hadi kukamilika kwake, ambapo watendaji mbali mbali wa sekta ...