NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WANAJAMII wametakiwa kuwa makini katika suala la kutoa ushahidi mahakamani, kwani ndio unaoweza kumtia hatiani mshitakiwa au kumuachia huru. Azungumza na wananchi wa Daya shehia ya Mtambwe Kusini, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Wete Maulid Hamad Ali alisema, ushahidi ni kitu muhimu katika kesi, hivyo kuna haja ya kutoa ushahidi kwa kina pale unapohitajika. Alisema kuwa, kuna makosa mbali mbali yanayotendeka katika jamii ikiwemo ya udhalilishaji, wizi na madawa ya kulevya, hivyo wasipokuwa makini katika kutoa ushahidi, washtakiwa wataendelea kuachiwa huru huku wanajamii wataendelea kulalamika. ‘’Ushahidi ndo ambao utamtia mshtakiwa hatiani au kuachiwa huru, kwa sababu unaangaliwa uzito wa ushahidi, hivyo tuwe makini tunapokwenda mahakamani kutoa ushahidi,’’ alisema Hakimu huyo. Aidha aliwataka vijana kuacha kutumia madawa ya kulevya kwani yanasababisha kujiingiza katika mambo maovu ikiwemo kuiba na hatima yake kuishia chuo cha mafunzo. Alisema kuwa, v