NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WANAKISOMO cha madarasa ya Elimu ya watu wazima kisiwani Pemba wameiomba Wizara pamoja na wafadhili kuwasaidia miwani, ili waepukane na usumbufu wakati wa kusoma na kuandika. Walisema kuwa, madarasa hayo ambayo kwa asilimia kubwa ni wanafunzi watu wazima, wakati mwengine wanashindwa kusoma wala kuandika kutokana na kupungua kwa nuru ya macho. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika vijiji tofauti, ikiwemo Mjinikiuyu shehia ya Minungwini Wilaya ya Wete,wanakisomo hao walisema wana shauku ya kujifunza zaidi ingawa wakati mwengine inawapa wakati mgumu kuhudhuria darasa. Walisema kuwa, kuna haja kwa Wizara ya Elimu pamoja na wafadhili wengine kuwasaidia kwa kuwapatia miwani, ili wahudhurie darasani wakiwa na hamasa ya kusoma na kuandika kwa bidii. Mmoja wa wanafunzi hao Viwe Yusuf Malik mwenye miaka 70 alieleza kuwa, anahudhuria darasa siku zote walizopangiwa lakini inapofika wakati wa kuandika ama anapoambiwa asome kwenye ubao macho yanamsumbua sana. &q