NA HAJI NASSOR, PEMBA:: MADEREVA wa vyombo vya moto kisiwani Pemba, wamewataka wanafunzi wa skuli, kutodharau honi wanazowapigia au mingurumo maalum ya mshine, ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika. Walisema, wanafunzi waliowengi wamekuwa na tabia ya kudharau honi au mivumo isiyokuwa na kawaida, wanayoifanya ili wakae pembeni, jambo ambalo linaweza kuleta madhara. Wakizungumza na mwandishi wa habari eneo la Ngwachani, ambapo dereva mmoja aliyekataa kutaja jina lake, alipoteremka kwenye gari, kuwaeilimisha wanafunzi waliodharau honi aliyowapigia mara tatu. Alisema, alilazimika kuweka gari pembeni, na kuwapa maneno makali kundi la wanafunzi, baada ya kuwapigia honi na mivumo mikali ya mashine, bila ya kujali. Dereva huyo alieleza kuwa, alikuwa amebeba mzingo akitokea bandarini Mkoani, na alipofika karibu na njia ya Tangaani, aliwapigia honi wanafunzi, ili wakae pembeni, ingawa hawakutii. ‘’Mbele yangu kuna gari mbili za abiria zinafukuzana zikitokezea mjini Chake chak...