Na Nihifadhi Abdulla, UNGUJA. Jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa siku hadi siku kuhakikisha usawa wa kijinsia unachukua nafasi yake kwa kupitia mikataba ya kimataifa, kikanda, sera, sheria, matamko na mbinu nyengine tofauti Mpango wa utekelezaji wa beijing katika maelezo ya dhamira namba 7 imeeleza uezeshaji wa mwanamke na ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa kuangalia uwiano wa jinsia ili kuhakikisha wanawake na wanaume wanapata nafasi sawa ya kushiriki katika ngazi zote za maamuzi Aidha Mkataba wa kikanda wa nchi za kusini mwa afrika kifungu cha 12 kinasisitiza ushiriki sawa wa wanawake kufikia asilimia 50/50 kwenye nyanja za maamuzi, pia kifungu namba 13 kinaeleza kuwekwa mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi na upigaji kura na kuondosha mila na desturi potofu zinazopingana na maendeleo ya mwanamke katika siasa na uongozi Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar ni taasisi inayotetea mambo mengi ya haki ikiw
IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA DIWANI wa Wadi ya Kiuyu Pemba kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Nasra Salum Mohamed amesema, atahakikisha anatatua changamoto zote zinazowakabili wananchi ili kuleta maendeleo katika wadi yake. Alisema kuwa, ametatua changamoto mbali mbali na anaendelea kushirikiana na wananchi kuziibua changamoto nyengine ili zipatiwe ufumbuzi kwa ajili ya maslahi yao na Taifa kwa ujumla. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika wadi yake alisema, baadhi ya changamoto alizotatua ni pamoja na kuhamasisha kujengwa vyumba vinne vya madarasa katika skuli ya Minungwini na vyumba vinne katika skuli ya maandalizi Kangagani. Mambo mengine aliyoyatatua Diwani huyo ni kuchimba shimo la vyoo (chamber) katika skuli ya Minungwini, kuezeka vyumba viwili vya skuli ya Mjinikiuyu, kujenga matundu manne ya vyoo katika skuli ya tutu Penjewani na ujenzi wa kituo cha Afya Minungwini. Diwani huyo alisema pia alitatua changamoto ya umeme katika kijiji ch