NA HAJI NASSOR, PEMBA:
MAHAKAMA
maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, imemkumkuta na hatia ya
ubakaji, wa mtoto wa miaka 4, mtuhumiwa Edson Saymon Shija ‘mtuhumishi’ miaka (42) wa Machomane
Chake chake.
Mahakama hiyo chini ya
Hakimu wake Muumini Ali Juma, ilisema, hayo yanajiri baada ya wiki mbili
zilizopita, upande wa mashataka, kukamilisha na kufunga ushahidi wao.
Alisema, mashahidi wote
watano walioletwa mbele ya mahakama hiyo, na kisha kuongozwa na Wakili wa
serikali, ilitosha kuonesha kuwa, mtuhumiwa huyo anahusika moja kwa moja.
Alisema, kwa ushahidi wa
awali na kwa kiasi ikubwa umeishawishi mahakama hiyo, kuamini kuwa mtuhumiwa
huyo, alimbaka mtoto wa miaka minne.
‘’Mshitakiwa, unanifahamu
kuwa, kwa ushahidi wa awali uliotolewa mahakamani hapa, na upande wa mashataka,
umekukuta na hatia, sasa unatakiwa ujipange ili uutie doa ushahidi
huu,’’alisema.
Hakimu huyo, alimfahamisha
mtuhumiwa huyo, njia tatu ambazo anaweza kuzitumia kwa ajili kufanya utetezi,
ikiwemo ya kiapo, bila ya kiapo na kukaa kimnya mahakamani hapo.
‘’Njia ya kukaa kimnya
upande wa mashataka hauwezi kukuliza suali, njia ya kiapo mahakama unauzingatia
na kisha utaulizwa maswali, ingawa bila ya kiapo hauzingatiwi sana na huulizwi,’’alimueleza Hakimu mtuhumiwa huyo.
Baada ya maelekezo hayo
kutoka kwa Hakimu, mtuhumiwa alichangua
njia ya kula kiapo, na kueleza kuwa, kwa siku ya jana hakuwa tayari kujitetea.
‘’Mimi nimechagua njia ya
kujitetea kwa njia ya kiapo, ingawa sio leo, maana siko vyema kiafya, naiachia
mahakama inipangie siku nyingine,’’aliomba mtuhumiwa huyo.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo,
aliahidi mahakamani hapo kuwa, siku itakayoamuliwa, atawasilisha mashahidi
wawili mbali ya yeye mwenyewe.
Mwendesha mashataka wa
serikali Ali Amour Makame, alidai kuwa hana pingamizi na uamuzi wa mahakama, na
wa mtuhumiwa wa kujitetea kwa njia ya kiapo na kutumia mashahidi.
Hivyo Hakimu Muumini Ali
Juma wa mahakama hiyo, bada ya kushauriana na upande wa mashtaka, alilipangia
shauri hilo kurudi tena mahakamani hapo, Novemba
21, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa
huyo Edson Syamon Shija ‘mtumishi’ (42), alidaiwa kumbaka mtoto
wa miaka minne (4), tukio lililotokea
Septemba 30, mwaka huu saa 2:00 usiku Machomane Chake chake.
Kufanya hivyo ni kinyume, na
kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6
ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment