NA HAJI NASSOR, PEMBA:::: JESHI la Polisi mkoa wa kusini Pemba, litampandisha mahakamani wakati wowote, Mwalimu skuli ya Msingi ya Madungu wilaya ya Chake chake Pemba, Ali Makame Khatib, akidaiwa kumchezea sehemu zake za siri na kisha kumbaka, mwanafunzi wake wa darasa la tano skuli hapo. Taarifa za Jeshi hilo, zilizotolewa na Kamanda wa Jeshi hilo mkoani humo, Abdalla Hussein Mussa alisema, kwa sasa wanaendelea kumuhoji mwalimu huyo, kuhusiana na tuhuma zinazomkabili, na kisha taratibu zikikamalika atafikishwa mahakamani. Alieleza kuwa, awali walipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa mama mzazi wa mtoto huyo, akidai mtoto wake, amechezewa na kisha kuingiliwa na mwalimu wake. Kamanda huyo alieleza kuwa, baadae taratibu za kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, zilifuata na kuanza kuhojiwa juu ya tuhuma hizo. Awali mama mzazi alidai kuwa, aligundua tatizo hilo kwa mtoto wake, baada ya kusikiliza moja ya kituo cha redio kikielezea aina za udhalilishaji. Mama huyo alieleza kuwa, mtoto wake ...