NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Makombeni wilaya ya Mkoani Pemba, wamesema bado wanahitaji elimu zaidi ya athari za utiririshaji maji machafu katika makaazi yao, ili kujiepusha na magonjwa ya kuharisha na kutapika. Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika shehiani hapo, walisema bado wapo baadhi yao wamekuwa wakitiririshaji maji hayo, bila ya kujalia afya za wenzao. Walieleza kuw, inawezekana wanaofanya jambo hilo ni kutokujua athari za maji hayo kwa jamii na hasa watoto ambao tahadhari yao ni ndogo. Mmoja kati ya wananchi hao Ali Khamis Juma alisema, moja ya chanzo cha utirirshaji wa maji hayo, ni magonjwa kama ya tumbo la kuharakisha na kutapika. ‘’Ni kweli suala la uchafuzi wa mazingira hasa la utiririshaji maji machafu lipo kwenye shehia yetu, na inawezekana wengi wao hawajui madhara,’’alieleza. Nae Semeni Juma Kheir, alisema hayo yanajitokeza kutokana na kutokuwepo kwa adhabu kali kwa wananchi wanaodharau uchimbaji wa shimo la kuhifadhi maji ...