NA KHAULAT SULEIMAN ,PEMBA WAZIRI wa Kilimo Mali Asili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis amesema Wizara imeandaa maonyesho nane nane kwa dhamira ya kuimarisha kilimo kwa dhana za kisasa pamoja na kuimarisha kilimo hai kwa manufaa ya bidha katika jamii ili kutoa fursa kwa tasisi za kiserikali na hata binafsi na wajasirimali na wananchi wote kwa ujumla. Serikali kupitia wizara ya kilimo mali asili na mifugo imekamilisha matayarisho yote ikiwa lengo ni kuhamasisha wakulima kutumia njia bunifu za kilimo cha kisasa na kuongeza uzalishaji na mbinu bora za kisasa katika kukuza pato la taifa kwa ujumla. Aliyasema hayo kwa wandishi wa habari huko katika ofisi za Wizara ya Kilimo Wete Jodari mkoa wa kaskazini Pemba wakati wa ghafla ya ufunguzi wa maonyesho ya kilimo ya nane nane ambayo yanafanyika Dole Kizimbani wilaya ya Magharibi A Unguja. Wizara ya Kilimo Mali asili na Mifugo inaendeleza mipango na mikakati iliyoanzishwa na serekali katika kuendeleza sekta ya kilimo ili kuona nch...