Skip to main content

Posts

Showing posts with the label DINI YA KIISLAMU

WAMBAA, CHUMBAGENI KUFANYA MASHINDANI YA QUR-AN MWISHONI MWA MWEZI HUU

   NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JUMUIYA ya kuhifadhisha kur-an ya kanda ya Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, inakushudia kuendesha mashindako ya kanda, mwishoni mwa mwezi huu, na kuwaomba waumini wenye uwezo, kuiunga mkono jumuiya hiyo, kwa ajili ya zawadi za washindi. Hayo yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ustadhi Hassan Othman Khamis, kwenye mfululizo wa vikao vya maadalizi, vilichofanyika Chumbageni chini ya msaidizi mlezi wao, Abrhaman Mohamed Khamis. Alisema, tayari Jumuiya hiyo imeshafanya mashindano ya mchujo uliofanyika Machi 1, mwaka huu, hivyo sasa inatoa nafasi kwa kuandaa mashindano makubwa, mwishoni mwa mwezi huu. Alieleza kuwa, ni nafasi kwa wenye uwezo kushirikiana na Jumuia hiyo, kwa ajili ya kukitangaaza kitabu cha Allah (S.W) kupitia mfumo wa mashindanI kwa wanafunzi. Mwenyekiti huyo, aliwakumbusha wale wenye nia ya kuungana nao, kuwa mwenye kuchangia jambo jema hasa katika mwezi huu mtukufu wa ramadhan, Muumba ameshahidi malipo makubwa kw...