NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MASHEHA kisiwani Pemba, wameonya kutojishusisha na uuzaji wa ardhi, kwani sheria zinazosimamia ardhi, hazitambui nafasi yao, katika zoezi la awali la uuzaji ama ununuaji. Ushauri huo umetolewa leo Mei 25, 2024 , na Hakimu wa mahkama ya ardhi ya mkoa wa kusini Pemba, Abdalla Yahya Shamuuni, wakati akijibu maswali ya wananchi wa shehia ya Kukuu Kangani, wilaya ya Mkoani, kwenye mkutano wa wazi, uliondaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar, kupitia mradi wa upatikanaji haki, unaofadhiliwa na UN-WOMEN kupitia Umoja wa Ulaya ‘EU’. Alisema, sheria ya Ardhi, zinaanza kutambua kazi ya sheha wa eneo husika, lililouzwa ardhi, wakati wa uhaulishaji, ambapo hapo yatahitajika maoni yake, pamoja na ya Mkuu wa wilaya. Alieleza kuwa, ni kosa kwa sheha, kujihusisha na mauziano ya ardhi, ingawa hutakiwa kuwepo kama shahidi, ili kuwa na taarifa sahihi zinazoendelea katika eneo lake. ‘’Sheha hahusiki moj...