NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ MPIRA wa kikapu ‘basketball’ ni aina ya mchezo unaochezwa sehemu nyingi duniani. Kwani kama ilivyo michezo mingine, nao huimarisha afya, huleta ajira, huondosha ubaguzi, na kuunganisha watu wa aina mbalimbali. Mchezo huu ni wa pili kwa umaarufu, baada ya mpira wa miguu kwa kupendwa na mashabiki wa michezo nchini, ambao wengi walicheza skulini na kupata wafuasi wengi. Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, mchezo huu ulianzishwa na Mwalimu James Naismith, kwenye chuo cha Springfield College huko, Massachusetts mwaka 1891. Alibuni mchezo huu kwa ajili ya wanafunzi wake, ili wapate mazoezi wakati wa kipupwe waliposhindwa kucheza nje, ambapo kwa mara ya kwanza, ulichezwa Disemba 21 mwaka huo huo 1891 nchini Berlin. Mpira wa kikapu, ulienea haraka ndani na nje ya vyuo vya Marekani, katika karne ya 20, ambapo mwaka 1936 mchezo huu ulikubaliwa kwenye michezo ya Olimpiki. Shirikisho la mpira wa kikapu duniani ‘FIBA’ na chombo cha usimamizi wa mpi...