NA ZUHURA JUMA, PEMBA WADAU wa habari kisiwani Pemba wamesema, kuwepo kwa baadhi ya vifungu vya sheria visivyo rafiki kwa wanahabari vinasababisha kunyima uhuru wa vyombo vya habari nchini. Wakizungumza wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya wadau juu ya maboresho ya vifungu vinavyominya uhuru wa habari, uliofanyika TAMWA Pemba, wadau hao walisema, kuna haja ya kuwekwa sheria ambazo zitawasaidia waandishi wa habari kufanya kazi zao bila vikwazo. Walisema kuwa, habari ni muhimu sana na ndio chanzo cha maendeleo katika nchi, hivyo ni vyema vifungu vya sheria vilivyo na mapungufu vifanyiwe maboresho na visivyofaa viondoshwe kwa maslahi ya wanahabari na jamii kwa ujumla. "Kwa kweli baadhi ya vifungu vyetu vya sheria havipo huru kwa wanahabari kwa sababu upande mmoja wamepewa uhuru lakini upande wa pili unapokonywa, kwa hiyo sio rafiki vinahitaji kurekebishwa", walisema wadau hao. Said Rashid Hassan kutoka kituo cha Huduma za Sheria Pemba alipendekeza kuwepo kifungu kitakachom