Na Najjat Omar – Unguja. Wadau wa masuala ya kijamii na kijinsia wamekutana kwa pamoja kuzungumzia sera na sheria zinahusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na mapungufu yake. Mkutano huo ambao umeendaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Zanzibar –TAMWA uliokutanisha wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali za kijamii na kiserikali kujadili juu ya ufuatiliaji,utekelezaji na kutoa maoni juu sera na sheria zinahusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia kwa jamii hususan watoto. Takwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali inaonesha matukio hayo yameongezeka kutoka matukio 1,222 mwaka 2021 hadi matukio 1,360 mwaka 2022, ongezeko ambalo ni la matukio 138. Takwimu hizo zinaonesha kwamba kwenye matukio 1,361 yaliyotokea mwaka 2022, matukio 1,173 yalijumuisha watoto, 185 yalihusu wanawake na matatu yalihusu wanaume. Kwenye matukio 1,173 ya watoto, 889 walikuwa ni wasichana, huku 284 walikuwa ni wavulana. Akifungua mkutano huo Afisa miradi ...