NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ TIMU ya Wawi star, imejihakikishia kubakia ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba msimu ujao, baada ya jana kuichakaza Azimio SC kwa mabao 3-2, kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Ngere ngere Jeshini, majira saa 10:30 jioni. Kwa timu ya Wawi star, mchezo huo kwao ulikuwa na maana pana, ili wajihakikishie kubakia kwenye daraja hilo, hasa kwa vile mchezo unaofuata wataumana na Junguni anayesaka alama za lazima za kuongoza ligi hiyo. Katika mchezo wa jana, ambao uliohudhuriwa na watazamaji wengi, ulianza kwa kasi, huku kila timu ikiangalia ulipo udhaifu wa mwenzake, ili aondoke na alama tatu muhimu. Katika kuhalalisho hilo, Wawi star ilianza kuwafurahisha washabiki wake, mnamo dakika ya 15, pale mshambuliaji wao hatari Suleiman Seif ‘Madeo’ alipotikisa nyavu kwa bao la kwanza. Lakini Azimio SC, kwa vile walishaazimia ushindi, walisawazisha bao hilo, mnamo dakika ya 34, kwa shuti la mbali lililopigwa na mlinzi wao Salum Kazumar, na kujaa wavuni. Ingawa ‘Ma...