Skip to main content

Posts

Showing posts from March 5, 2023

WEJISA WAJUMUIKA NA WANAWAKE WENZAO KUSHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

  Na Mwandishi Wetu, WAFANYAKAZI wa Kampuni ya  Weka Jiji Safi Limited  (WEJISA ) wameungana na wanawake wenzao kusheherekea sikujui ya wanawake inayoadhimishwa Machi 8 Kila mwaka. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bi.Nuru  Hassan amesema kuwa, maadhimisho hayo yanaleta chachu ya Maendeleo kwa wanawake Kwa sababu ya Rais Samia Suluhu Hassan  kuonyesha njia ya kuwa wanawake tunaweza. Amesema kuwa Rais Samia ameweza  kuweka mazingira mazuri ya wanawake kujituma na kufanya kazi Kwa bidii bila ya kuwa wategemezi , jambo ambalo limeongeza uchapakazi Kwa jinsia hiyo. "Rais wetu Samia tunamuunga mkono kwa sababu nafasi aliyonayo amesaidia kuongeza mwamko kwa wanawake kufanya kazi na wale ambao walikua hawana kazi na kutafuta shughuli zozote ili waweze kujiondoa kwenye utegemezi," alisema Nuru. Alisema kuwa, kampuni ya WEJISA  itaendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega na ndo maana leo tumekuja hapa kusheherekea pamoja na kujifunza mengi kwa Wafanyakazi wetu Wanawake" alise

UWT YATOA ONYO KWA WANAWAKE UNYANYASAJI WATOTO

  NA MARYAM SALUM, PEMBA MWENYEKITI wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda amewataka wanawake wenzake kuacha tabia ya kuwanyanyasa   na kuwatelekeza watoto kwani hilo sio jambo la busara kwa jamii na hata mbele ya Mungu. Wito huo ulitolewa Machi 8, 2023 na Mwenyekiti huyo katika Kiwanja chakufurahishia watoto kilichopo Tibirinzi Chake Chake kwenye wiki ya siku ya mwanamke Duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo machi 8 ya mwaka. Alisema kuwa suala la malezi kwa   watoto sio la mzazi mmoja ni jukumu la kila mmoja ndani ya jamii ili kuondosha changamoto mbali mbali zinazoweza kujitokeza. Alieleza kuwa sio jambo la busara kwa mzazi kutupa mtoto ama kutelekeza mtoto kwa sababu tu yakukosa huduma ama mahitaji kutoka kwa mwenza wake. “Tusitupe watoto kwani hatujui hapo mbeleni mtoto huyo unaemtupa atakuja kuwa nani katika jamii, hivyo tulee watoto wetu kwa kila hali ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili wa Kijinsia ambao umeshamiri ndani ya jamii zetu,” alisema Mwenyekiti huyo. Alifaha

WIZARA YA ELIMU: ''WANAFUNZI WARIPOTINI WAALIMU WANAOWANYEMELEA KIMAPENZI''

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali wilaya ya Chake chake, imewataka wanafunzi kuwaripoti mara moja, waalimu watakaoonesha dalili za kuchupa mipaka yao ya ualimu, na kuelekea katika vitendo vya udhalilishaji dhidi yao. Kaimu Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali wilayani humo, Khamis Juma Yahya, alitoa agizo hilo leo Machi 8, 2023 wakati akizungumza na wanafunzi wa skuli ya sekondari ya Dk. Omar Ali Juma, kwenye kampeni maalum, ya kuongeza uwelewa, kwa wanafunzi wa skuli, madrassa, vyuo vikuu na klabu za sanaa, iliyoandaliwa na TAMWA-Zanzibar. Alisema waalimu nao ni binaadamu, kama walivyowengine, wanaweza kujisahau na kuanza kuvunja maadili yao, hivyo ikijitokeza hayo, wanafunzi wasisite kutoa taarifa za haraka. Alieleza kuwa, udhalilishaji hauna kabila, mtu maalum, umri, cheo wala wakati, hivyo wanafunzi hawanabudi kuwa makini na waalimu, ambao watawataka kimapenzi. ‘’Niwakumbushe jambo wanafunzi wangu, hata waalimu kwa vile ni binaadamu wanaweza

WAANDISHI WA HABARI PEMBA, WAPIGWA MSASA MTUMIZI YA TAKWIMU

      NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KAMISAA wa sensa ya watu na makaazi Balozi, Mohamed Haji Hamza, amesema baada ya matokeo ya sensa kutoka, anavitegemea sana vyombo vya habari, kuielezea jamii umuhimu wake. Kamisaa huyo aliyasema hayo Machi 7, 2023 ukumbi wa kiwanda cha Mafuta Makonyo Wawi wilaya ya Chake chake, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye mafunzo ya matumizi ya takwimu za sensa za mwaka 2022. Alisema, kwa vile jukumu moja wapo la vyombo vya habari ni kuelimisha, hivyo ni wakati sasa kutumia wajibu huo, kuwaeleza wananchi umuhimu wa takwimu hizo. Mapema Mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar Salum Kassim Ali, alisema ili nchi ipange mikakati na mipango thabiti ya maendeleo, takwimu ni jambo la msingi. ‘’Bila ya takwimu sahihi na kisha kutumika vyema, hakuna jambo ambalo litafanikiwa, liwe la maendeleo ya haraka au ya muda mrefu,’’alieleza. Kaimu Mtakwimu mkuu ofisi ya Pemba, Said Mohamed alisema serikali imetumia gharama kubwa, kufanikisha sensa ya watu na

DCU: TOWENI VIBALI VYA MIRADI HARAKA DK: MNGEREZA

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI        06/03/2023   DCU Toweni Vibali vya Miradi Haraka - Dkt Mngereza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Dkt. Mngereza Mzee Miraji ameitaka Kamati ya Udhibiti na Usimamizi Ujenzi (DCU) kutochelewesha kutoa vibali vya miradi ili ujenzi wa miradi hiyo utekelezwe kwa muda   uliyotakiwa. Dkt. Mngereza aliyasema hayo jana baada ya kupokea maoni ya wajumbe katika kikao cha 74 cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Baraza la Manispaa ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alisema maombi ya vibali vya miradi yasikae muda mrefu yawe yamejibiwa ili ujenzi wa miradi uanzwe kutekelezwa kwa wakati. Pia aliitaka kamati hiyo kuanzisha utowaji wa vibali vya ujenzi kwa njia ya mfumo wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia (ICT) ambapo utawezesha kamati hiyo kufanya majukumu yao ipasavyo. “Vibali vya miradi visikae muda mrefu havijatolewa, kuwe na time frame, pia kuwe na land forum, mfikirie kuanzisha mfumo wa ICT na

SMZ KUKOMESHA TATIZO LA OMBAOMBA

  Na Mwandishi Wetu:::::: WAPO  baadhi ya watu huwatumia watu wenye ulemavu kama ni mtaji wa kuwapatia kipato hali ambayo imechangia kuwepo kwa idadi ya ombaomba kwa watu wenyeulemavu Zanzibar. Kwa kuliona hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewaonya wenye tabia hiyo ya kuwatumia watu wenyeulemavu kwa shughuli zao binafsi ikiwemo za ombaomba watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya sheria. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na idara maalum SMZ Masoud Ali Mohamed, anasema  serikali inafahamu kuwepo kwa watu wanaowatumiya watu wenye ulemavu kwa ajili ya kujipatia kipato binafsi.  Waziri huyo anasema serikali inafahamu kuwepo kwa matukio ya aina hiyo ambapo tayari baadhi ya watu wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kuwatumiya watu wenye ulemavu. Anasema watu hao waliokamatwa wamekutwa wakiwahifadhi watu wenyeulemavu katika nyumba moja visiwani Zanzibar na huwasambaza katika maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar kwa ajili ya kuomba

WADAU WATAKA SHERIA ZINAZOGUSA TASNIA YA HABARI KUFANYIWA MAREKEBISHO, WASEMA ZIMEEGEMEA SERIKALINI ZAIDI

    NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIBAR KILA raia katika nchi hii anastahili kupata haki zake za msingi za kila siku awe mtu mwenye ulemavu au asiye na ulemavu, Mwanamke na mwanamme, watoto, wazee na vijana. Hivyo basi panapozungumzwa haki ni kwamba makundi yote yana haki katika jamii na taifa kwa ujumla. Kwa mfano katiba zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar zimezungumzia waziwazi haki za msingi kwa raia wote bila ya ubaguzi. Hivi karibuni Wanaharakati na wadau wa masuala ya habari walipitia baadhi ya sheria zinazohusiana na habari ikiwa ni pamoja na kuangalia, kujadili, kushauri na kupendekeza utendaji mzuri wa usimamizi wa mchakato mzima na mwenendo wa sheria zinazogusa vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla. SHERIA ZINAZOGUSA TASNIA YA HABARI Miongoni mwa sheria hizo ni kuangalia Mianya ya kisheria katika Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria No.8 ya 1997 sambamba n