NA KAIJE SALIM, ZANZIBAR@@@@ Wajasiriamali wameomba kupatiwa mitaji ili waweze kujikwamua kutoka katika hali moja ya kimaisha na kuelekea kwenye hali nyengine ya kipato cha juu. Ombi hilo limetolewa na wajasiriamali walioshiriki katika mafunzo yaliyo tolewa na SMIDA huko Maruhubi chuo cha utalii. Miongoni mwa washiriki hao ni Aisha Said Omar wameeleza wamekuwa wakishindwa kujikwamua kimaisha kutokana na mitaji midogo waliyonayo. Chales Silima kutoka kutoka Mamlaka ya mitaji na dhamana amesema wamekuja Zanzibar kutoa elimu ili wafanya biashara na wajasiri amali wapate kujiendeleza zaidi Amesema mafunzo hayo yatawawezesha hasa vijana kuanzisha majukwa yakujiendeleza kibiashara na kujiwezesha kufikia katika kuongeza kipato. Kwa upande wake mkurugenz mkuu Wakala wa maendeleo ya Viwanda vidogo na vyakati SMIDA Soud Said Ali amesema wataendelea kushirikiana wajasiri amali kwa kuwapatia mafunzo iliwapate kufanya kazizao za uzalishaji kwa usahi na kufikia malengo ...