Skip to main content

Posts

Showing posts with the label CCM CHAMBANI

CHAMBANI, WAZINDUZI KAMPENI BAHATI AAHIDI NEEMA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MGOMBEA Uwakilishi wa Jimbo la Chambani kwa tiketi ya CCM Bahati Khamis Kombo, amesema kama akipewa tena ridhaa ya kushika nafasi hiyo, atahakikisha anaendeleza alipoishia kwa miaka mitano iliyopita. Mgombea huyo uwakilishi aliyasema hayo leo Septemba 29 , mwaka huu uwanja wa mpira wa Dodo Pujini jimboni, kwenye uzinduzi wa kampeni kwa jimbo hilo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa Ilani ya CCM. Alisema aliamua kuomba tena nafasi hiyo, baada ya kuona bado anadeni la maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Chambani, katika huduma mbali mbali za kijamii. Alisema, CCM kila baada ya miaka mitano, imekuwa ikiwaletea Ilani, ambayo ndio mpango kazi mkuu wa utendaji wa kazi, na inatoa dira ya miradi kadhaa inayokusudiwa kutekelezwa. ‘’Hivi sasa CCM, imeshaleta tena Ilani kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025/2030 na ndani yake yamo miradi ya maendeleo, na ndio maana, naomba tena ridhaa kuyaendeleza hayo,’’alifafanua. Nae Mbu...