NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ JESHI la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, limekiri kupokea malalamiko ya mwanamke mmoja, akimtuhumu mtendaji wa Jeshi hilo, kumbaka ndani ya kituo cha Polisi. Jeshi hilo limesema, ni kweli walipokea lalalamiko hilo, ingawa lilisema ili kukamilisha na kutoa taarifa rasmi, wamo kwenye upelelezi. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Disemba 6 mwaka huu majira ya saa 8: 17, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mussa Mwakasula, alisema kwa sasa hawana taarifa pana juu ya tukio hilo. Alieleza kuwa, kwa sasa wanaendelea na uchunguuzi wa tukio hilo, na hasa baada ya kuzipata taarifa hizo, kutoka kwa mlalamikaji. ‘’Ni kweli tumepokea lalamiko la mwanamke mmoja, akimtaja askari wetu, kwamba ndie aliyembaka, ingawa kwa sasa taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguuzi wetu kukamilika,’’alisema Kaimu Kamanda huyo. Baadhi ya wananchi waliokataa kutaja majina yao , walisema mwanamke huyo kabla ya kudai kutendewa kosa hilo, alifika kituo cha Poli...