NA FATMA HAMAD, PEMBA MKURUGENZI wa Jumuiya ya Wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA, Jamila Mahamoud Juma, amezitaka asasi za kiraia, kushirikiana kwa pamoja na kuwajengea uwezo watoto wa kike, waliyokatisha masomo, ili waweze kurudi na kupata haki yao ya msingi. Mkurugenzi huyo, aliyasema hayo katika mkutano wa kuutambulisha mradi wa Malala, utakaoendeshwa na ZAFELA, Zanzibar kwa muda wa mwaka mmoja, kikao kilichowajumuisha asasi mbali mbali za kirai kisiwani Pemba. Alisema katika utafiti wao walioufanya, waligundu kuwa, kuna wimbi kubwa la watoto wa kike wamekuwa wakikatisha masomo yao, kutokana na sababu mbali mbali, ikiwemo kuolewa, kupata mimba za utotoni pamoja na kufanyishwa kazi za nyumbani. Alisema, wamekuwa wakipokea kesi nyingi za watoto wa kike, kudai haki zao, aidha waliolewa au waliojihusisha na mahusiano, ambao ukiwangalia umri wao unapaswa wawe wako masomoni. ‘’Tumeamua kuleta mradi huu wa ‘Malala’ kwa ajili ya kumuezesha na kumsaidia mtoto wa kike,