NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ZOEZI la uchukuaji wa fomu za kuomba ya kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi na viti maalum kupitia chama cha Mapinduzi ‘CCM ‘wilaya ya Chake chake, linaendelea vyema. Zanzibar leo ambalo lilifika ofisi ya CCM wilayani humo majira ya saa 2:00 asubuhi, liliwashuhudia wanaccm wakijitokeza mfululizo kuchukua fomu hizo, kwa nafasi kadhaa zilizotangaazwa. Mtinia wa kwanza kwa nafasi ya uwakilishi kutoka Jimbo la Chonga Ahmed Abubakar Mohamed, alifika ofisini hapo majira ya saa 2:40, na kufika chumba cha kwanza, kwa ajili ya usaili, kabla ya kukutana na Katibu wa CCM na kukabidhiwa fomu. Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi ya CCM mjini Chake chake, mtia nia huyo alisema, ameamua kuchukua fomu hiyo, ili kuunga nguvu za Rais wa sasa wa Zanzibar, ya kuwaletea maendeleo wananchi. Alisema, amekuwa akivutiwa mno na kasi ya Dk. Mwinyi jinsi anavyowafanyia wananchi wake maendeleo, na ndio maan...