NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ WAZAZI wanawake wa kijiji cha Jamvini shehia ya Ndagoni, wilaya ya Chake chake Pemba, wametakiwa kutenga muda wa kukaa na watoto wao, ili kuwaonesha njia za wao kuwa viongozi mapema, ikiwa ni pamoja na kuwalea bila ya ubaguzi. Ushauri huo umetolewa na Masaidizi wa sheria Jimbo la Ziwani, shehia ya Wesha Khadija Said Khalfan, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwenye mfululizo wa mikutano ya kutoa elimu, inayoratibiwa na Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake ‘CHAPO’. Alisema, njia moja wapo ambayo inafaa kuafutwa kwa wazazi hao, ni kuacha ubaguzi wa malezi kama vile kubagua kazi ndani ya familia zao. Alieleza kuwa, kazi kama za kwenda dukani, kushughulikia mifugo, kubeba kuni zinatakiwa zisitolewa kwa ubaguzi, bali watoto wa kike wafanyishwe, ili kukataa dhana ya ubaguzi. Msaidizi huyo wa sheria alieleza kuwa, njia nyingine ambayo inaweza kuwatayarisha watoto wa kike kuwa viongozi wa baadae, ni