NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ALIYEKUWA Mratibu wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba, ‘CHAPO’ Mohamed Hassan Abdalla, amechaguliwa kwa kura za ndio, kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Jumuiya hiyo, iliyokuwa wazi. Mahamed Hassan, ambae hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo mdogo na wa dharura, alijizolea kura 15 kati ya kura zote 17 zizopigwa na wanachama wa CHAPO. Akitoa matokeo hayo leo Augost 31, 2024, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya 'CHAPO' Hafidh Abdi Said, alisema wapiga kura wote, walitarajiwa wewe 23, ingawa hadi muda wa kupiga kura unafika kulikuwa na wajumbe 17 pekee. Alieleza kuwa, kwa mujibu wa katiba ya CHAPO, imeanisha idadi ya wajumbe wote, ni kufikia nusu, ili kufanya uamuzi iwe wa uchaguzi ama kupitisha ajenda. ‘’Idadi ya wanachama hai 17, kati ya 23 haijakikua katiba ya 'CHAPO' na ndio maana, tumefanya zoezi la uchaguzi na mshindi ambae ni Mohamed Hassan Aballa, kwa nafasi ya Mkurugenzi ameshinda,’’alifafanua. ...