NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ ‘HAMASA kubwa ilifanyika tokea pale ilipoanzishwa timu ya Mkoani Queens mwaka 2014 na hadi sasa kuweza kusimama’. ‘Pamoja na dharau, kejeli ambazo tumepewa lakini bado tunaendelea mbele kuhakikisha timu yetu inakata mawimbi na kusonga mbele’. Ni kauli ya baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu wanawake Mkoani qunes, walipokuwa wakizungumza na makala haya kuhusiana na uhai wa timu yao. Timu hiyo iliyoanzishwa mwaka huo wa 2014, ikiwa na wachezaji 26, imepitia madhila makubwa kwa jamii husika ila bado inaonekana kuwepo. Wanasema pamoja na wanajamii kuwachukulia wanawake wanaocheza soka, wanafanya uhuni wao hawakujali hilo, maana nia walikuwa wanaijua wenyewe. Wachezaji hao wanatumia fursa ya vipaji vyao kuhakikisha wanaingiza kipato na kuhudumia familia zao, kujiajiri na kufanya mambo mengine ya kimaendeleo kutokana na kipato wanachopata kupitia vipaji vyao. Mmoja wa muanzilishi wa timu hiyo ambae sasa ni kocha wa timu hiyo ya ...