NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika uzinduzi wa tamasha la 31 la utamaduni wa mzanzibari, linalotarajiwa kufanyika leo hii, uwanja wa michezo Gombani Chake chake Pemba. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika, kuanzia majira ya saa 8:00 jioni ya leo, na shamara shamara na maandalizi ya tamasha hilo zitaanzaa mapema, uwanjani hapo. Akizungumza na mwandishi wa habari, Kamishna wa Utamaduni Zanzibar Dk. Omar Salum Mohamed alisema, maandalizi yote yameshakamilika, kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha hilo. Alisema kuwa, lengo kuu la kuanzishwa tamasha hilo, ni kuhakikisha wazanzibari wanaendelea kukumbushwa, kuelimishwa na kushajiishwa, kuzingatia mila silka, desturi, maadili na mambo mengine yote yanayohusu utamaduni wao. "Katika tamasha hili hapa kisiwani Pemba mchana wa leo, tunatarajia sana, kuwa mgeni rasmi awe Rais wetu wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, maana...