NA MWANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WAVUVI wa bandari ya Tanda Tumbi Shehia ya Mjanaza Wilaya ya Micheweni Pemba, wametakiwa kufuata maelekezo yanayotolewa na mamlaka ya Hali ya Hewa, ili kuweza kujikinga na matatizo yanayoweza kutokea wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi. Hayo yalielezwa na Mkaguzi wa Polisi ambae pia ni Polisi shehia ya shehia ya Mjanaza Khalfan Ali Ussi, wakati akikabidhi simu kwa wavuvi hao, ikiwa ni ahadi iliyoitoa kwao hivi karibuni. Alisema, kwa vile wao ni wavuvu anamatumaini makubwa kuwa, simu hizo lengo lake ni kuwasaidia katika shughuli zao hizo, pindi wanapopatwa na majanga mbali mbali. Alifahamisha kuwa, lengo la kutoa simu hizo ni kutokana na maafa mbali mbali, ambayo yanawapata wavuvi wakiwa katika shughuli zao, na kukosa chombo cha mawasiliano. "Leo (jana), nimekuja kwa ajili ya kutimiza ahadi yangu, niliyoiweka kwenu kuwapatia simu ambayo itaweza kuwasaidia, pindi mnapotokezea kadhia yeyote ile wakati mkiwa katik