NA NUSRA SHABAN@@@@ WAWANAWAKE katika nafasi za uongozi wanakutana na changamoto mbalimbali zinazohusiana na usalama wao. Changamoto hizo zimekuwa sehemu ya hali halisi inayowakumba wanawake wengi ambao wanashika madaraka, haswa katika muktadha wa kijamii na kisiasa. Katika historia ya Zanzibar, wanawake walikuwa na nafasi ndogo katika maeneo ya uongozi lakini hivi sasa walau idadi ya wanawake viongozi imeongezeka tofauti na miaka ya nyuma. Mfano hai mwaka 2010, Tanzania iliweza kupata wanawake wabunge 23 waliopata nafasi zao kupitia majimbo ya uchaguzi. Ukijumuisha na wale wa viti maalumu, Bunge la Tanzania likafikisha asilimia 29 ya wabunge wanawake -kiwango cha juu kabisa kwa wakati huo. Kadhalika, 2020 zilifanyika Chaguzi tatu katika ngazi ya Ubunge na Udiwani ambapo katika chaguzi hizo, jumla ya Wabunge wanawake 73 walishinda chaguzi hizo na kuchaguliwa kuwa Wabunge wa Majimbo huku upande wa Madiwani Jumla ya Wanawake 654 wakichaguliwa kuwa Madiwani katika Shehia husika. Kat...