Skip to main content

Posts

Showing posts from May 1, 2022

MOTIVATE STUDENTS TO INCREASE PERFORMANCE IN NATIIONALI EXAMS

BY HAJI NASSOR, PEMBA Suleiman has recently completed secondary school education at Mikindani Dole School in Unguja West ‘A’ District. He was among 20 students who scored Division One in the 2021 National Certificate of Secondary Education Examinations (CSEE). The results impressed teachers, parents and education stakeholders because it was the first time such performance was attained since the school was established. Although the school was not one of the top 10 schools listed in the examination results nationally, Mikindani was one of the top 10 schools in the isles. However, this success was not realized by accident but it was attributed to students zeal and teacher-to-student motivation, according to the School Head Master, Rajab Ali Issa. He said the school administration recognized and honored all the students who passed their exams with flying colours, adding, “We rewarded all the students who scored Division One in their national exams” he said. He said ‘the top s

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MHADHIRI CHUO KIKUU HURIA TANZANIA AWAPA DARSSA WAZAZI, WALEZI PEMBA

:  MHADHIR wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ‘OUT’ tawi la Pemba, Sheikh Bakari Kombo Bakari, amesema waumini wa dini ya kiislamu, wanao wajibu wa kuendeleza mafunzo waliyoyapata katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kivitendo. Amesema isitoshe kwa waislamu, kuona kwamba mwezi wa Ramadhani umemalizika na kuacha ibada mbali mbali walizokuwa wakizitekeleza kipindi hicho cha mfungo, kwani itakuwa ni sawa kama vile walijizuia kula na kunywa katika wakati huo. Mhadhiri huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu waliohudhuria kwenye mahafali ya sikukuu ya Eid al-fitri, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar na kufanyika msikiti wa Makonyo Wawi Chake Chake. Alisema ni wajibu ya wazazi na walezi, kuwalea watoto wao katika maadili ya uisalamu, na kuwabidiisha kufanya ibada ikiwemo kuswali, kusoma Qur-an na kutoa sadaka kwani ndiyo mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W). ‘Vijana wetu wengi wameacha ibada na badala yake wamekuwa wakijishughulisha na mambo ya kip

WANAONYIMWA, KUCHELEWESHEWA MIRATHI PEMBA WAONYESHWA NJIA

NA HAJI NASSOR, PEMBA MWANASHERIA wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar ofisi ya Pemba, Massoud Ali Massoud, amewataka wanawake, wanaonyimwa au kucheleweshewa mirathi, kuitumia Kamisheni hiyo, ili kupata ufumbuzi wa haraka. Alisema, wanawake wamekuwa ndio waathirika wakubwa, pale familia zinapochelewesha kurithi, ama wakati mwengine kutorithi kabisa, hivyo Kamisheni ni sehemu muhimu kwa waathirika kama hao. Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika Samail Gombani Chake chake, na kuyashirikisha makundi ya wanawake na watu wenye ulemavu, alisema sio busara kwa wanawake kuendelea kukoseshwa haki zao. Alieleza kuwa, ni wakati sasa kwa jamii za kiislamu kuitumia Kamisheni hiyo, kwa ajili ya kupata ushauri na mamna bora ya kufanya shughuli za mirathi. ‘’Sasa wananchi wanaotaka kufanya mirathi waje ofisini kwetu, maana hata lile tozo, limeshuka kutoka asilimia 5 kabla ya mwaka 2008 na sasa kufikia asilimia 0.25,’’alieleza. Akatolea mfano kuwa, kwa sasa mirathi yenye thamani ya shilin

WAANDISHI WA HABARI WAWEZA KUWA DARAJA LA WASIO NA SAUTI IKIWA......

NA ZUHURA JUMA,PEMBA KILA ifikapo Mei 3 ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari. Siku hiyo waandishi hupata nafasi ya kujadili mazuri na mabaya wanayokumbana nayo katika kitumiza kazi ya kikatiba ya kuwapa habari wananchi. Zipo tasisi kabla ya kufikia kilele hicho, huwa na shughuli mbali mbali kama vite matembezi katika maeneo wanayochukua habari au mikutano ya pamoja. Kwa upande wa Klabu ya waandishi wa habari Pemba , PPC wao walikuwa na shughuli ya kongamano la siku moja lililofanyika Gombani Chake chake kisiwani humo. Kongamano hilo lililowashirikisha waandishi wa habari, wahariri na wadau mbali mbali, kwa lengo la kuhakikisha kwamba kuna uhuru wa vyombo vya habari. Ilitajwa kuwa, vyombo vya habari ni daraja muhumu katika jamii, ambalo husaidia kupata habari na taarifa mbali mbali, kutoka kwa watawala na jamii wenyewe. Mabadiliko hayo huletwa kwa njia mbali mbali kama vile kuelimisha, kushajihisha, kuelekeza na kujenga ushawishi wa mambo ambayo

WIZARA YA AFYA PEMBA YATOA TAMKO KUSHIKILIWA DAKTARI WAKE

NA HAJI NASSOR, PEMBA. WIZARA ya Afya Pemba, imekiri kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, kwa mfanyakazi wake ambae ni daktari wa kituo cha Afya Gombani Chake chake. Kaimu Afisa Mdhamini wizara huyo Pemba, Yussuf Hamad Iddi, alisema ingawa sio rasmi, lakini baada ya kufuatilia wamebaini kuwa hajaacha kazi, bali anashikiliwa kwa tuhma za kutorosha na ubakaji. Alisema, ingawa taarifa za kesi hizo zaidi ziko kituo cha Polisi, lakini wanajua kwa sasa, mfayakazi wao huyo Is-haka Rashid Hadid, hayupo kazini kwa muda. ‘’Ni kweli mfanyakazi wetu ambae ni daktari katika kituo cha Afya Gombani wilaya ya Chake chake, alichukuliwa na Polisi, akiwa kazini, kwa tuhma za utoroashaji na ubakaji wa mtoto,’’alieleza. Katika hatua nyingine, aliwataka watendaji wa wizara hiyo kisiwani Pemba, kuendelea kuheshimu maadili na sheria za kazi, ili kutoa huduma kwa uhakika. Aidha alisema, kwa sasa wanaendelea kufuatilia hatua kwa hatua juu ya mwenendo wa kesi hiyo, licha ya kutokupok

ZSSF PEMBA YAWAPA TATIMA 60 SIKUKUU

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA. MFUKO wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ‘ZSSF’ kisiwani Pemba, umekabidhi sadaka ya fedha taslim, kwa watoto yatima 60 kisiwani humo, kama sehemu ya maandalizi ya kusherehekea sikukuu, baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Akikabidhi sadaka hiyo kwa nyakati tofauti, Meneja wa ZSSF kisiwani humo, Rashid Mohamed Abdalla, alisema ZSSF inapaswa kuihudumia jamii, wakiwemo watoto waliokosa wazazi wao. Alisema, ZSSF imeguswa mno na kundi la watoto hao, na dio maana imeamua kwa mara hii, kuacha kufutarisha makundi mengine na kuwapatia sadaka watoto hao. Akiungumza katika ofisi za wilaya za Micheweni, Wete, Mkoani na ofisini kwao Chake chake, alisema ijapokuwa, sadaka hiyo ni ndogo, lakini itasaidia katika maandalizi ya sikukuu. Alieleza kuwa, watoto hao ambao wamepoteza mmoja kati ya wazazi wao, au wote wawili, nao wanahitajia kupata furaha na chukula kizuri hasa kipindi cha sikukuu. ‘’Kwa msimu huu ZSSF makao makuu, imeamua kuacha kuyaita makundi mengin

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

JAA LA KIBELE ZANZIBAR LILIVYOGEUKA KISIMA CHA AJIRA

  IMEANDIKWA NA ALI SULEIMAN, PEMBA KIJIJI cha Kibele kipo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar. Kwa mujibu sensa ya watu na makazi ya 2012, kijiji hiki kina watu wasiopungua 3,000. Wengi wao wanajishughulisha na kilimo. Hapa ndipo lilipo jaa kuu la Unguja, ambalo linatumika kukusanyia taka zinazozalishwa majumbani, masokoni, madukani, barabarani na kwenye hoteli za kitalii. Jaa hili lipo umbali wa mita 300 kutoka barabara kuu iendayo Wilaya ya Kusini. Wastani wa tani 190 za taka mchanganyiko kama za plastiki, tairi mbovu, televisheni na majokovu yasiyofaa kwa matumizi, zinatupwa katika jaa hili kila siku. Aidha hili ndio eneo linalotumika kuharibu dawa au vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binaadamu. Vingi ya vifaa vya elektroniki ninavyoviona katika jaa hili ni vile vilivyoingizwa kutoka ng’ambo kama biashara chakavu. Eneo hili lina ukubwa wa zaidi ya mita 1,000 sawa na viwanja 10 vya mpira. Ukifika hapa, unapokelewa rundo la taka zilizotawanyika huku harufu kali ya uvundo ik

MOHAMED KHATIB KHAMIS, MJASIRIAMALI ANAENDESHA MAISHA YAKE KWA UFUGAJI NYUKI, ANA MIZINGA 75

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA: SASA ni saa 5:40 asubuhi, nipo pembezoni mwa nyumba ya mjasiriamali wa ufugaji nyiki, hapa kijiji cha Kidutani shehia ya Chumbageni, wilaya ya Mkoani Pemba. Nilichukua dakika 35 kwa gari binafsi, kutoka katikati ya mji mkuu wa Pemba Chakechake, hadi hapa anapoishi mjasiriamali huyu. Mohamed Khatib Khamis miaka 46, kwa sasa anaishi katika nyumba ya miti, mbele ya nyumba yake ameshusha baraza, ndogo alioijenga kwa miti na mabaki ya mbao. Hapa anayobiashara ndogo ya viazi mbatata, vitunguu, mchele na sukari, ametengeneza mabao mithili ya daraja, hutumia kiti cha plastiki rangi ya bluu kuwasubiri wateja. Hapa Kidutani, wapo wengine ni wafanyakazi serikali, ingawa kazi kubwa ya wakaazi wa eneo hili nimearifiwa, ni kilimo cha migomba, mihogo, michungwa na minazi. Wapo wengine wakiwa na mashamba makubwa ya mikarafuu, na wachache wasiozidi watano, wamejiajiri kama alivyo mwenyeji wangu Mohamed Khatib Khamis. Safari yangu wala haikushia hapo kwenye makaaz

WANAWAKE, WATOTO HAWAJAFIKIWA IPASAVYO NA ELIMU YA VVU, UKIMWI

NA ZUHURA JUMA, PEMBA: ………..KUNI ya akiba daima huicheka inayoteketea jikoni……bila ya kujua kuwa ikimaliza nayo itafuata…………..   Kauli hii ya wazee wa zamani, ndio inayotoa tawira kwa viongozi wa leo ambao huwacheka wanawake na watoto jinsi wanavyokumbwa na changamoto kwenye maambukizi mapya ya VVU na Ukimwi. Kumbe wanasahau kwamba, watoto ni kuni zilizojikoni na zinateketea na zikimalizika sasa ni zamu ya waliowakuwa wakichekelea na kuwaona watoto na wanawake hawahusiki kupewa taaluma ya ukimwi. Mimi naamini watoto wa Tanzania, kama walivyo watoto wengine ulimwenguni kote, nao wana haki ya kuzaliwa wakiwa huru bila ya kuwa na VVUna ukimwi. Watoto hao ambao hutajwa kuwa ndio taifa jipya na viongozi wetu wa kesho, wanaopaswa kulindwa ili kuhakikisha hawaambukizwi na VVU, ambapo matokeo yake hukubwa na magonjwa mengine. Kwa Tanzania bado suala la elimu ya Ukimwi limekuwa likiguswa kijumla jumla ambapo makundi hatarishi kama ya watoto, wanawake na makundi mengine hayazingati