NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KATIBU Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, amewakumbusha wakuu wa vitengo vya wizara hiyo Pemba, kuendelea kufanyakazi kwa pamoja, kwani huo ndio msingi wa mafanikio. Alisema, changamoto ya udogo wa bajeti ya kutosha, uhaba wa watendaji katika vitengo vyao, pamoja na kikwazo cha usafiri, vinaweza kupata ufumbuzi, ikiwa wataendelea kufanyakazi kwa ushirikiano. Katibu Mkuu huyo, aliyasema hayo Gombani Chake chake, wakati akisalimiana na wakuu wa vitendo vya wziara hiyo, alipokuwa kisiwani Pemba, kwa mapunziko ya sikukuu. Alieleza kuwa, umoja na mshikamano ndio suluhisho la changamoto kadhaa zinazowakabili, na kinyume chake, wanaweza kuyumba kiutendaji. Alifahamisha kuwa, kama viongozi wakuu wa wizara hiyo wanashirikiana kwa karibu, ni vyema mwenendo huo wakauiga, kwani unaweza kuwapandisha juu kiutendaji. ‘’Niwalazimishe watendaji wenzangu, kuwa mkitaka kufanikiwa pamoja na changamoto kadhaa, jambo la...