NA HAJI NASSOR, ALIPOKUWA BEIJING WAANDISHI wa habari wa mataifa ya Afrika, wameiomba serikali ya China, kuyapa mataifa yao miradi endelevu mikubwa ya maendeleo, ili baadae yaweze kujiendesha, badala ya kutegemea misaada kila baada ya muda. Wakizungumza kwenye ziara ya kuvitembelea vituo vya Tehema, star times vilivyopo Beijing nchini China, walisema urafiki na uhusiano wa China na mataifa ya Afrika, unaweza kuchapuzwa na miradi mikubwa. Mwandishi wa habari kutoka Gambia Arret Jatta, alisema kwa muda mrefu mataifa hayo, yamekuwa yakipokea misaada kutoka kwa serikali ya China, ingawa baada ya miradi kumazilika, hurejea kwenye utegemezi. Alieleza kuwa, China imekuwa ikitumia mamiliobi ya dola, kuyaunga mkono mataifa ya Afrika, ingawa huwa ni kwa kiasai kidogo, kwa mujibu wa mahitaji ya wakati uliopo. ‘’Wakati umefika sasa kwa taifa la China, kulielekea taifa moja moja la Afrika, na kulipa msaada mkubwa wa maendeleo, katika nyanja ama ya elimu, afya, miundombinu ili...