NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WATUHUMIWA wa kesi ya kuua kwa makusdi, inayowakabili vijana wanne akiwemo Ali Mussa Omar ‘Mkapa’ na wenzake, wote wakaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake, wamerejeshwa tena rumande, baada ya Jaji anayesikiliza kesi yao kutokuwepo mahkamani. Watuhumiwa wingine waliorejeshwa rumande hadi Januari 23, 2024 ni Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 na Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, ambao wanatuhumiwa kumuua kwa maksudi kijana Said Seif Kombo. Mara baada ya kuwasili mahakamani hapo wakitokea rumande, walitulia tuli wakisubiri taratibu za mahakama kuu ziendelee, ingawa Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Awamu Zubeir Awamu, alidai kuwa Jaji husika hayupo mahakamani hapo. Wakili huyo wa serikali, alimueleza hakimu wa mahkama ya mkoa Chake chake anayeshughulikia makosa ya udhalilishaji Ziredi Abdull-kadir Msanifu, juu ya dharura ya Jaji husika wa kesi hiyo. ‘’Mheshimiwa Hakimu, ilikuwa kesi hii...