NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ ‘’HESHIMA, bidii ya kazi, upole, ustahamilivu na kufanya uamuzi sahihi, ndio njia moja wapo za kuwatumikia watu,’’anasema Mkuu wa wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki. Anasema inawezekana waliowengi, wandhani ili uwe kiongozi mzuri, lazima uchupe mipaka, kimavazi, heshima, uondoe upole, ukiuke sheria, jambo ambalo ni tofauti. Anahadithia wakati wakiwa mtendaji wa Tume ya Uchaguzi, miaka 15 iliyopita, alichunga sana nidhamu na heshima yake, huku akihakikisha halazi kazi. Alizingatia mno kivazi cha heshima, kujenga mapenzi ya kazi kwa kila mmoja, na kuhakikisha kitengo chake hakifeli kwa jukumu, walilopewa. ''Kuna wakai tunasafirisha vifaa tena siku ya mvua, ilipofika majira ya saa 5:50 usiku, wapo walionitaka nirudi nyumbani kumpunzika na wao wataendelea na kazi, niligoma,''anakumbushia. Aliwaambia kama ni wakati wa kazi wanafanya kwa pamoja na wakati wa kumpunzika, wanapumzika kwa pamoja, maana kazi ndio kazi. ‘’Siku hiyo kila mmoj...