NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ WADAU wa habari kisiwani Pemba, wametakiwa kutumia taaluma zao katika kuelimisha jamii kuhusu maendeleo yalioyopatikana ndani ya awamu ya nane ya Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Hussein Ali Mwinyi. Hayo yalielezwa jana Juni 21, 2025 na Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Rashid Hadid Rashid kwenye kongamano la wadau wa habari, lililofanyika katika ukumbi wa "ZRA" Gombani Chake chake Pemba. Alisema ipo haja ya wanahabari kutumia taaluma zao vizuri, ili kuimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wananchi, hasa zinazohusu maendeleo, kutokana na umuhimu wa taarifa hizo. Alieleza kua serikali ya awamu ya nane chini ya Raisi Dk. Mwinyi imepiga hatua kubwa za maendeleo katika kuwasogezea huduma bora wananchi wake, ya maeneo mbali mbali ya mjini na vijijini. "Serikali ya awamu ya nane, imepiga hatua kubwa katika maendeleo nchini kwa kuwasogezea huduma mbali mbali, hivyo ni vizuri wa...