ZUHURA JUMA NA HAJI NASSOR, BEIJING@@@@ WAANDISHI wa habari wa nchi za Afrika, wametakiwa kuendelea kujifunza lugha mbali mbali, ili kusaidia kukuza uchumi katika mataifa yao. Akifungua mafunzo ya siku 20 katika Ukumbi wa Hoteli ya RoyalLink ZiYu, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (CICG) Han Likiang alisema kuwa, kujua lugha mbali mbali ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo kuna haja kwa wanahabari kujifuza zaidi. Alisema kuwa, ili uchumi ukue unahitaji mambo mbali mbali ikiwemo waandishi wa habari kujifunza lugha ambazo zitawasaidia kuandaa makala, vipindi na habari zenye tija hususan zinazogusa viashiria vya ukuaji wa uchumi wa ndani. ‘’Watakapotumia lugha mbali bali itawasaidia kuwahabarisha watu wengi duniani ambao wanaweza kuvutia hata wawekezaji na wageni, ambayo ni miongoni mwa kukuza uchumi wa ndani,’’ alisema. Akizungumzia umuhimu wa CICG kuandaa mafunzo hayo ni kuendeleza uhusiano wa kimataifa wa china na mataifa mengine ya Afrika kwa lengo...