NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT- Wazalendo Othman Massoud Othman, amesema kama akipata ridhaa ya kuingoza Zanzibar, atasimamisha utawala wa sheria na haki, ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza uchumi. Alisema, haiwezekani wananchi kupata maendeleo endelevu, kama hakuna utawala wa sheria, ambao utawahakikishia wananchi kubaki na mali zao ikiwemo ardhi. Mgombea huyo wa urais wa aliyasema hayo jana Septemba 18, 2025, uwanja wa mpira wa Mpika tango Mkoani, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho, wa kampeni. Alisema, utawala huo wa sheria, utakuwa na mambo kadhaa, ikiwemo kila mmoja kupata heshima ya kufanya shughuli zake, kwa mujibu wa sheria. Alieleza kuwa, kufanya hivyo ni kuifungua Zanzibar kiuchumi, kutokana na watu kuheshimiana na kutunza amani na utulivu miongoni mwao. ‘’Kama nikiingia mdarakani, nitahakikisha, kwanza tunakuwa na utawala wa kuheshimiana, ambao ndani yake utamuhakikishia kila mmoja ma...