Skip to main content

Posts

Showing posts from June 21, 2026

TAMWA YAWAPA MAFUNZO YA UWAJIBIKAJIN MADIWANI NA WARATIBU WANAWAKE

NA MOZA SHAABAN, PEMBA MADIWANI wakuchaguliwa na waratibu wanawake na watoto kutoka wilaya nne za Pemba   wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika utekelezaji majukumu yao ya msingi ya kiuongozi, ili kujenga imani kwa jamii juu ya uwezo alionao mwanamke katika kuongoza na kuleta maendeleo. Wito huo umetolewa na Afisa Progamu wa mradi wa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika masuala ya uongozi (SWIL) unaotekelezwa na TAMWA-Zanzibar Sabrina Ali Mwatanga wakati wa mafunzo   kwa madiwani na waratibu wanawake na watoto kutoka wilaya nne za Pemba, yaliolenga kuwajengea uwezo juu ya namna ya kuwajibika ipasavyo katika uongozi wao, yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano TAMWA Mkanjuni Chake chake Pemba. Alieleza mafunzo hayo ni mwendelezo wa hamasa na kuwajengea uwezo madiwani na waratibu hao juu namna bora ya kutekeleza majukumu yao ya kiongozi, ili jamii ione ufanyaji kazi wao kivitendo. Afisa huyo alisema   TAMWA imekua ikifanya juhudi kubwa katika kuwajengea uwezo wana...

CANADA YAKABIDHI VIFAA VYA SH/= MILION 270 VYA UCHUMI WA BULUU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ SERIKALI ya Canada, imesema itaendelea kushirikiana na serikali za Tanzania, katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kwenye uchumi wa buluu, ili walengwa wakuze pato lao na taifa. Hayo yameleezwa leo Juni 23, 2026 na Balozi wa taifa hilo, nchini Tanzania Emily Burns, kwenye hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa vikundi vya wajasiriamali, waliokeza kwenye bahari, na ufunguzi wa kituo cha mafunzo eneo la Chamanangwe wilaya ya Wete Pemba. Alisema, ushirikiano huo, anaamini utawasaidia wajasriamali waliokeza kwenye eneo hilo, hasa wanawake na vijana, ambao kwa muda mrefu walikuwa hawakuhusishwa moja kwa moja. Alieleza kuwa, kwa eneo la Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania bara, ilivyozungurukwa na bahari, wakati umefika manufaa yake, yawanufaishe makundi yote. ‘’Serikali ya Canada, inaziahidi serikali zote mbili kwamba, ushirikiano huu kwenye sekta ya uchumi wa buluu, utakuwa endelevu pamoja na maeneo mingine,’’alifafanua. Katika hatua nyingine, B...