Skip to main content

Posts

Showing posts from November 20, 2022

WAZIRI RAHMA ASITISHA UJENZI KITUO CHA 'WATER SPORTS' ZANZIBAR

    Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Rahma Kassim Ali amesitisha ujenzi wa michezo ya baharini (Water Sports) unaojengwa na Muekezaji NJ Water sports eneo la fukwe za bahari Matemwe Wilaya ya Kaskakazini ‘A’’ kwa madai ya kukiuka kanuni na sheria ya Ardhi. Agizo hilo amelitoa mara baada ya kufanya ziara katika eneo hilo ambalo linadaiwa kuwa na mgogoro wa ardhi baina ya Muekezaji NJ Water Sports na Matemwe Bangaloes ambapo kesi ya mgogoro huo imeshafikishwa Mahakama ya Ardhi Gamba Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja. “Nimelazimika kusitisha ujenzi unaoendelea ili kuweza kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ikiwa ni msimamizi mkuu wa masuala ya ardhi" sitoweza kuacha ujenzi uendele wakati kesi iko mahamani alisema Waziri huyo.   Alisema Mahakama ya Ardhi Gamba imeshatoa   maamuzi ya kusimamisha ujenzi wa muekezaji NJ Water Spots   ambae anadaiwa kuingia eneo la mwekezaji mwenzake huko Matemwe. Alifahamishwa kwamba Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya

VIONGOZI WA DINI PEMBA 'WAFOK'A WATOTO WENYE ULEMAVU KUFUNGIWA NDANI

  HAJI NASSOR, PEMBA::: VIONGOZI wa dini kisiwani Pemba, wamewakumbusha wazazi na walezi, kuwafichua na kuwasajili watoto wao wenye ulemavu, ili wajiunge na wenzao, kama njia ya rahisi ya kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu. Walisema, wazazi na walezi wanaowajibu wa kuhakikisha watoto wao wote wanapata haki za msingi kama elimu, matibabu bora, haki ya kucheza ili kutanua upeo wa ufahamu wao. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya mchango wa viongozi wa dini, katika kuihamasisha jamii ili kundi la watu wenye ulemavu, kupata haki zao, walisema kwanza ni kuwatoa nje. Mmoja kati ya viongozi hao sheikh Issa Hassan Maalim wa Chake chake alisema, kumfungia ndani mtoto kwa sababu ya ulemavu wake, ni kosa. ‘’Suala la ulemavu ni kudura ya Muumba, sasa kama mzazi anaichukulia kama ni kosa na kuamua kumfungia ndani, anamdhalilisha mtoto wake,’’alieleza. Nae kiongozi wa kidini nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Aisha Hasnuu Omar, alisema wazazi wote wanalojukumu la

KISA CHA MWAKA PEMBA ''MUME WANGU HAJAMBAKA MTOTO WANGU WA KAMBO''

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: SHEMSA Hakim Khamis wa Chanjamjawiri wilaya ya Chake chake, ameiambia mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini Pemba kuwa, mume wake hajambaka mtoto wao wa kumlea, bali ni uongo alioutengeneza mtoto huyo.   Alidai kuwa, mtoto huyo amekuwa muongo mzoefu na mzushi, maana siku ambayo, alidai amebakwa na mumewake, alikuwa safarini kikazi kisiwani Unguja.   Shemsa ambae ni shahidi nambari nne kwenye shauri linalomkabili mumewake (mtuhumiwa Said Abdalla Issa ), alidai kuwa mumewa alikuwa kisiwani Unguja kikazi siku hiyo aliyodaiwa kubaka.   Alidai kuwa, mtoto huyo ambae ni wa kulea, amekuwa muongo na alishawahi kumsingizia jirani wao mwanamme, kuwa alishawahi kumvulia nguo na kumuonesha sehemu zake za siri, ingawa walipofuatilia, haikuwa sahihi.   Mke huyo wa mtuhumiwa, alidai kuwa mtoto huyo pia alishawahi kukamatwa na barua ya mahaba, ndani ya mkoba wake wa mabuku ya skuli, akiashiria kuwa mtoto huyo alishaanza kubadilika kit

BILALI WA VITONGOJI RUMADE TUHUMA ZA UBAKAJI

    NA HAJI NASSOR, PEMBA:::: MTUHUMIWA Bilali Hamad Kombo miaka 19, mkaazi wa Vitongoji wilaya ya Chake chake mkao wa kusini Pemba, ameanza kuhemea rumande, akikabiliwa na tuhma za kumbaka mtoto wa miaka 14.   Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha mashataka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa mashataka Ali Amour Makame kuwa, mtuhumiwa huyo bila ya halali na bila ya ridhaa ya wazazi wake, alimtorosha na kisha kumbaka mtoto huyo.   Alidai kuwa, tukio la kwanza la utoroshaji lilitokea Oktoba 29, mwaka huu, majira ya saa 1:40 asubuhi ambapo, mtuhumiwa anadaiwa kumtorosha mtoto huyo kutoka nyumbani kwao na kumpeleka nyumbani kwake Vitongoji wilaya ya Chake chake.   Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (a) cha sheria Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.   Kosa la pili linalomkabili mtuhumiwa huyo, ni la ubakaji, kwa mtoto huyo huyo, alilodaiwa kulitenda pia Oktoba 29, mwaka huu, majira ya saa 2:00 asubuhi, wakati akiwa naye nyumbani kwake. Kufany

WAZAZI WA WATOTO WENYE ULEMAVU PEMBA WANAKIU YA POSA.....

  HAJI NASSOR, PEMBA:: WAZAZI na walezi wa watoto wenye ulemavu shehia ya Vitongoji wilaya ya Chake chake Pemba, wameitaka jamii kutowabagua vijana wao, kwani wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa, ili kuanzisha familia. Walisema, bado baadhi ya familia zimekuwa haziwachagua watoto wao kike, kwa sababu ya ulemavu wao, jambo ambalo wanasema ni kuwanyima haki zao masingi. Wakizungumza kwenye mkutano wa kuihamasisha jamii kutiii sheria na kufanyika Vitongoji, walisema wamekuwa na watoto wa kike kwa muda mrefu, bila ya kugongewa mlango. Mmoja kati ya wazazi hao Omar Khamis Omar, alisema jamii haiwaoni vijana wenye ulemavu kama sehemu ya kuanzisha familia, jambo ambalo linawatia unyonge. Alisema imekuwa ni adimu kuona mtu mwenye ulemavu anaolewa au wakati mwengine kukubaliwa posa yake, jambo ambalo, linawazidishia kujiona wanyonge. ‘’Mimi nna mwanangu ana ulemavu wa viungo, basi tulienda kupeleka posa baba mzazi akakubali, ingawa baada ya familia kukutana, tukirejeshwa kwa sababu

ALIYEMLAWITI MTOTO WA MIAKA 9, AFUNGWA MIAKA 20 PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:: KIJANA Massoud Khamis Mussa wa Vitongoji wilaya ya Chake chake, kuanzia Novemba 15 mwaka huu, ataendesha maisha yake akiwa chuo cha mafunzo, kwa muda wa miaka 20, baada ya mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, kumtia hatiani, kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 9. Mahakama hiyo chini ya Hakimu wake Muumini Ali Juma, ilisema imefikia uamuzi huo, baada ya mashahidi watano waliowasilishwa mahakamani kutoa ushahidi, ambao uilikidhi vigezo husika. Hakimu Muumini alitumia dakika 35 kumsomea hukumu mshitakiwa huyo, ambapo alisema ushahidi nambari moja ambao umetia hatiani mshitakiwa huyo, ni ule uliotolewa na mtoto wa miaka 9. Alisema mtoto huyo, wakati anatoa ushahidi wake, aliithibitishia mahakama kuwa, mshitakiwa Massoud Khamis Mussa, ndie mtu pekee ambae alishawahi kumlawiti akiwa bandani kwake. ‘’Mtoto alisema kuwa, siku ya kwanza kabla ya kulawitiwa, mshitakiwa alitumia mafuta ya nazi, kuupaka uume wake na kisha nae kumpaka

WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM PEMBA WAIPA NENO SERIKALI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: WANAFUNZI wenye mahitajia maalum katika skuli mbali mbali kisiwani Pemba, wameikumbusha serikali kuzidi kuimarisha miundo mbinu ya kielimu, ili watimize haki yao ya kupata elimu kwa ufanisi.     Walisema, bado serikali imekuwa ikiweka mikakati zaidi kwenye maandishi, ingawa hawaoni utekelezaji wake hasa kwa baadhi ya skuli, na kuendelea kuwaacha wao wakiwa kwenye mazingira magumu.   Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi   kwa nyakati tofauti, wasema wameshaitikia wito wa kwenda skuli kuungana na wenzao kutafuta elimu, ingawa bado wamezungurukwa na cgangamoto.   Mmoja katia ya wanafunzi Abdalla Hussein skuli ya Tumbe, alisema ukosefu wa vitabu vya nukta nundu, waalimu wenye utaalamu ni moja ya changamoto zinazowakabili.   ‘’Bado mazingira ya sisi wenye mahitaji maalum katika skuli skuli zetu hayajakuwa rafiki kwa sisi wenye ulembu wa aina mbali mbali, ni wakati wa serikali kuimarisha,’’alileza.   Nae mwanafunzi Asha Hil

'MTUMISHI' KUJITETEA LEO TUHMA ZA KUMBAKA MTOTO MIAKA 4

    NA HAJI NASSOR, PEMBA:: MAHAKAMA maalum ya makosa ya udhalilishaji mkoa wa kusini Pemba, asubuhi hii inatarajia kusikiliza utetezi wa mtuhumiwa Saymon Shija ‘ mtuhumishi’ miaka (42) wa Machomane Chake chake, anayedaiwa kumbaka mtoto wa miaka 4.   Mahakama hiyo chini ya Hakimu wake Muumini Ali Juma, ilisema, hayo yanajiri baada ya wiki mbili zilizopita, upande wa mashataka, kukamilisha na kufunga ushahidi wake.   Alisema, mashahidi wote watano walioletwa mbele ya mahakama hiyo, na kisha kuongozwa na Wakili wa serikali Ali Amour Makame, ulitosha kuonesha kuwa, mtuhumiwa huyo anahusika moja kwa moja.   Alisema, kwa ushahidi wa awali, kwa kiasi ikubwa umeishawishi mahakama hiyo, kuamini kuwa mtuhumiwa huyo, alimbaka mtoto wa miaka minne (4).   ‘’Mshitakiwa, unanifahamu kuwa, kwa ushahidi wa awali uliotolewa mahakamani hapa, na upande wa mashataka, umekukuta na hatia, sasa unatakiwa ujipange ili uutie doa ushahidi huu,’’alisema.   Hakimu huyo, alimfahamisha mtuhum

TAMWA -ZANZIBAR YAWAKUMBUSHA JAMBO WANAMTANDAO PEMBA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::: CHAMA cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar, kimewataka wanamtandao wa kupinga matendo ya ukatili na udhalilishaji kisiwani Pemba, wasikatishwe tamaa, kwa kuibuka kwa matendo hayo kila siku, ni ishara wananchi wapeta uwelewa.   Hayo yameelezwa na Afisa Tathmini na ufuatiliaji kutoka TAMWA-Zanzibar Mohamed Khatib, kwenye kikao cha siku moja cha kuwasilisha ripoti ya utendaji kazi wa wanamtandao hao, kilichofanyika mjini Chake chake. Alisema kazi kubwa imeshafanywa na inaendelea kufanywa na wanamtandao hao, na ndio maana katika siku za hivi karibuni, wanaodhalilishwa wamekuwa wakieleza. Alieleza kuwa, ongezeko la takwimu ya matendo hayo pamoja na wanaotendewa na hata watu wao wa karibu kuripoti, ni dalili kuwa, sasa jamii imepata mwamko. Afisa huyo aliwataka wanamtandao hao, kutokatishwa na tamaa na ongezeko la matendo hayo, ambapo hilo linatokana na matumizi sahihi ya kuifikisha elimu. ‘’Hivi sasa mtoto anadhalilishwa na baba y

SHUMBA MJINI PEMBA WATUMIA MAJI YA BAHARI KWA MATUMIZI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA WANANCHI 6,680 wa shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba, wanakabiliwa na huduma ya maji safi na salama isiyo ya uhakika kwa mwezi mmoja sasa, unaowapelekea baadhi yao, kutumia maji ya bahari kwa shughuli zao za kila siku.   Walisema, huduma hiyo imekuwa ya kusua sua katika baadhi ya vijiji vyao, hali inayowanyima usingizi, huku baadhi yao, wakinunua kwa dumu moja lenye ujazo la lita 20, kati ya shilingi ya 500 hadi shilingi 1,000, kutoka shehia jirani.   Wananchi hao wa vijiji vya Chamboni, Vumbini, Nduaga, Momogu, Mkunguni, Kichekwani, Tundumwe na Msasani kwa wale wasio na uwezo wa kunua huduma hiyo, wamekiri kutumia maji ya bahari, kwa shughuli nyingine.   Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, walisema maji wanayonunua hutumia kwa ajili ya kupikia na kunywa na kukoga tu, ambapo kwa upande wa shughuli za chooni na kukoshea vyombo, hutumia maji ya bahari.   Mmoja kati ya wananchi hao Hamad Ali Hamad, alisema sio wote wenye uwezo