Skip to main content

Posts

Showing posts with the label KOCHA WA NETI BOLI WETE

BIMKUBWA: MUANZILISHI MPIRA WA PETE WETE, AELEZEA ALIVYOPAMBANA NA DHANA POTOFU

    NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ ‘TULIANZISHA  mchezo huu tukiwa tunajiamini huku  tukijuwa  kuwa na sisi wanawake tuna haki ya kujishirikisha katika michezo ya aina mbali mbali’.    Hayo ni maneno ya kocha wa mpira wa pete timu ya Mchanaga mdogo Center Bimkubwa Maulid Othman, aliyezungumza na makala haya.   Kocha Bimkubwa aliyasema maneno hayo huko katika maeneo ya skuli ya Mchangamdogo Wilaya ya Wete Kisiwani Pemba, ambapo ndipo wanapofanyia mazoezi.   Akinisimulia miongoni mwa sababu ya kuanzisha mchezo huo, ni pamoja na kuwa michezo ni ajira, afya na kupata kujuwana na watu.    Ingawa anasema alianza kuupenda mchezo huo tokea akiwa mwanafunzi na alikushaanza kuucheza ila kuna kipindi, alisita japo kama ndoto yake ni kuwa mwanamichezo.   Anasema kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo jamii kuwadharau na kuwaona hawafanyi kitu cha maana, na kudai michezo si kwa wananwake, ilibidi avunjike moyo na kukaa tu.   “Tokea tuanzi...