NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ MKUU wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika mashindani ya tano ya tahafidhil-quran, ya kanda ya Wambaa wilayani humo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa Jumuiya ya tahafidhil qur-an kanda ya Wambaa, Mwalimu Abdalla Haji Ali, alisema tayari maandalizi ya shughuli hiyo, yameshakamilika. Alisema, mkuu huyo wa wilaya, atawashuhudia wanafunzi wakishindana kwa juzuu ya kwanza, pili, tatu, tano, saba, 10 na 15 wakiwemo wanafunzi wa kike na kiume. Alieleza kuwa, mashindani hayo ya aina yake kwa mwaka huu, yanatarajiwa kufanyika msikiti wa Ijumaa, uliopo kijiji cha Chumbageni Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba. Alisema, baada ya majaji kukamilisha kazi yao hiyo na kutoa matokeo, mgeni rasmi huyo atatoa zawadi ikiwemo fedha taslimu, kwa washindi na washiriki wote 42. āāNi kweli asubuhi hii, ndani ya msikiti wa Ijumaa Chumbageni, mkuu wetu wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakari, atayashuhudia mashindani y...